Along Mwai Kibaki Road

Saturday, April 14, 2012

Dress hii inapatikana kwenye UK size 10 na 12






2 comments:

Anonymous said...

KWANI MKISEMA VIMETOKA CHINA NANI ATAKATAA?? VITU VINAONEKANA HIVI HIVI NI VYA CHINA MNASEMA MADE IN USA REALLY...BE HONEST TO YOUR CUSTOMERS.

Vazi said...

Sisi TUNAKUPENDA kwa sababu hatuna SABABU ya Msingi ya kukuchukia wewe, au mtu ambaye hajatutendea ubaya, wala hajafanya uhalifu kwa mtu yeyote.


JIBU LETU KWAKO WEWE TU PEKE YAKO NA SI KWA WATEJA WETU WENGINE MNAOSOMA SASA (Nyinyi Mafashionista ni waelewa pengine kuzidi hata Vazi)

kwanza: Tunauza nguo kwa kuzingatia kuwa mteja anatumia PESA, MUDA, na UPENDO Wake Kutufikia Vazi. Na Hatufanyi Biashara ya Mtu anunue, say Dress Vazi Leo anavaa mara moja akiweka kwenye maji limeshaharibika, AU Hawezi kutamani kuivaa tena. Mteja akinunua nguo ikawa hivyo hawezi tena kurudi dukani.

Tunapenda MTEJA akinunua nguo VAZI iwe ya mtoto au ya mtu mzima, aifurahie yeye, kwa muda mrefu na wanaomuona kaivaa wafurahie pia, ili pesa na MUDA WAKE alioutumia Vazi Viwe vimetumika Vizuri. "VALUE FOR MONEY".

Tunafanya kazi Hii kwa "passion"
Kinachotufurahisha zaidi kwanza ni mtu aridhike na afaidi kwa muda mrefu, bidhaa anayoinunua Vazi. Kwa sababu ukiwa kinyume na hapo mtu atarudi tu na nguo aliyoinunua na kulalamika. " Hivi kama ni wewe anony 12:13 utajisikiaje? kama unauza nguo, tena after 2 days mtu anarudi analalamika? Sisi Vazi haijawahi kutokea na ingetokea ingetuumiza Sana. Ndio Sababu tunakuwa Makini na Nguo tunazoweka dukani LAZIMA kuwe na Uhusiano kati ya Bei na Quality.


TATU: Hii ni Blog: Huwezi kurusha picha tu bila kuandika chochote pembeni ya hiyo picha inapooza sana. MADE IN USA iliyokupa shida hadi ukafanya maamuzi ya kusema "we are not honest" kama ni made in USA, utakuwa unakosea, cse hizo nguo za MADE IN USA bado zipo dukani na unaweza kufika dukani UKASOMA LABEL ukaondoa huo wasiwasi.




NNE: Tunakuhakikishia kwamba vazi tuna hofu ya Mungu wazungu wanaita " Fear of God" Kudanganya ni jambo linaweza kutuumiza sasa kisaikolojia kwa hiyo HATUWEZI KUDANGANYA WATEJA. Uongo ni Chukizo Mbele za Mwenyezi Mungu ambae anatuona popote tulipo, na Uongo ni Chukizo kwa Mungu, ambaye tunamtegemea atuongoze katika biashara na katika Maisha kwa ujumla.

tukisema MADE IN USA, Hiyo nguo kweli ni MADE IN USA. Pia tunapenda kukufahamisha kuwa HATA Nguo za CHINA ni Nzuri hata Hao Madesigner Wakubwa duniani wanaouza nguo zao mpaka $ 650 = 1,040,000/ Ya Kitanzania au bei zaidi ya hapo, wanatengeneza nguo zao CHINA na zinaandikwa MADE IN CHINA. Kwa Hiyo Hiyo isikupe shida. Naamini wengine wapenda Fashion Hili mnalijua SANA. Vile vile kuna vitu MADE IN TANZANIA na ni vizuri(mf. Khanga za Urafiki, unavaa zaidi ya Mwaka na Haipauki)

TANO: Haya maelezo ni kwa ajili ya anonymous aliyecomment 7 12:33)
Watanzania Wanajua Nguo SANA Akiishika tu "TEXTURE" M'BONGO kashajua Hii nguo ni ya Ukweli au poor quality. Kwa hiyo si rahisi kuweka nguo zenye poor quality Bongo halafu ukasema ni High Quality na ukaweka bei ikilingana na High Quality, Kwa bongo, haitawezekana. Ndio maana kuna Magauni ya 18,000 mshono na rangi ni uleule na ya 170,000/= mtu anatoa 170,000/- anaiacha ya 18,000/ kwa sababu akizishika kwa pamoja zote mbili anaona tofauti.

Hayo ndio majibu yetu kwako, Nadhani umetuelewa, ila kuna baadhi ya WATU Wanakuwaga NEGATIVE bila hata kutaka kufahamu zaidi kwa chochote wanachokiona, ila pia ni vizuri next time ukiwa na wasiwasi unatupigia tunazungumza na kueleweshana zaidi. Ukitaka Ushahidi wa RISITI za Maduka ya MAREKANI, SWEDEN NA UINGEREZA tunakonunua Nguo na Bidhaa zingine za vazi Tutakuonesha. Kufika Dukani tumia Google Map(ramani) inaelekeza tulipo.